Jengeni tabia ya kutembea kwa
Miguu Safari Fupi -
Bw Sekirasa..
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewataka wananchi wanaotumia usafiri wa barabara hasa jijini Dar es Salaam,kujenga utaratibu wa kutembea kwa miguu kwa safari fupi ili kupunguza msongamano wa magari.
Akizungumza katika mkutano wa mamlaka hiyo na madiwani wa Halmashauri tatu za Jiji la Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra,Israel Sekirasa(Pichani)alisema msongamano wa magari hautokani na magari ya abiria (daladala),tu bali pia magari ya watu binafsi.
Bw Sekirasa alisema wakati serikali kupitia taasisi zake na wadau mbalimbali wakifanya jitihada za kupunguza tatizo hilo,jamii inapaswa kuunga mkono kwa kupunguza baadhi ya matumizi ya magari yasiyo ya lazima kama hayo ya kutembea kwa miguu kwa safari fupi.“Nchi inakabiliwa na tatizo la msongamano,lakini si hilo tu,bali hata tatizo la nishati,jambo linalosababisha kila kukicha nauli kupanda,hivyo ni wakati wa kushirikiana sote kupunguza tatizo hilo kwa kuepuka kupika ovyo kwa kutumia mkaa na mafuta ya taa,”alisema.
Aidha aliushauri uongozi wa Jiji,mbele ya Naibu Meya Ahmed Mwilima aliyekuwa mgeni rasmi, kuandaa ziara ya madiwani katika Halmashauri ya Mji wa Moshi kujifunza mbinu walizotumia kuweka mji huo safi na nidhamu ya madereva katika kauli,sare na nauli.Mwilima alisema suala la ziara mjini Moshi litafanyiwa kazi na halmashauri husika ili kuona kama mbinu walizotumia zinaweza kusaidia katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.Habari hii na Gloria Tesha/TSN
No comments:
Post a Comment