Mbunge Anne Kilango
awaka Tena..
Mheshimiwa Mbunge,Anna Kilango
----------
Kama ilivyo ada yake juu ya kupambana bila woga na vitendo vyote vinavyoashiria ufisadi, Mbunge wa Same Mashariki,Mheshimiwa Anne Kilango Malecela (CCM),amewaka tena Bungeni leo na kuibana Serikali ili ieleze kwa kina juu ya hatua iliyofikiwa katika kuwafuatilia wale wote waliozoa mkopo wa Sh.Bilioni 216 na kisha kutozirejesha Serikalini.
Pesa hizo ni zile za mfuko wa mkopo maalumu wa kuwezesha uagizaji wa bidhaa kutoka nje nchi, yaani Commodity Import Support(CIS),ambazo zilikopwa na baadhi ya wafanyabiashara na kutorejeshwa tangu mwaka 1992 na hivyo Mheshimiwa Kilango akataka kujua ni hatua zipi zimeshachukuliwa katika kufuatilia suala hilo.
Mhe.Anne amesema anashangaa kutosikia lolote juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali,kwani mwezi April,Serikali ilitoa muda wa miezi mitatu kwa wakopaji wa mapesa hayo wawe tayari wamesharejesha.Bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment