Friday, July 25, 2008

Sikukuu ya Mashujaa leo jijini
Dar es Salaam...
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga washiriki wa hafla hiyo ya kuwakumbuka mashujaa
Leo jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete leo alishiriki katika kutoa heshima kwa mashujaa waliopigania Tanzania kwa kuweka silaha za asili na maua kwenye mnara wa kumbukumbu za mashujaa uliopo katika Viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini mbalimbali nchini.Katika hafla hiyo Rais Kikwete aliweka Mkuki na ngao,Sime,Shada la maua,upinde wa mshale pamoja na shoka tukio ambalo pia liliwahusisha viongozi wa mabalozi nchini,mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Abdul Kimbasa na mwenyekiti wa Tanzania legion.

Pia viongozi wa dini ya kiislamu,wakristo na Wahindi walikuwepo kuwaombea dua mashujaa hao.Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam mizinga miwili ilipigwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa hao.Habari na Mdau Msimbe Lukwangule.

No comments: