Monday, July 28, 2008

SALAAM ZA PONGEZI KWA JESHI LA
POLISI NCHINI...

S
-------------
Ninawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya khs uhalifu ambao umekuwa ukitokeza mara kwa mara, Najuwa mnafanya kazi ktk mazingira magumu sana,hamna vitendea kazi,muhimu, pia na familia zenu zinaishi maisha ya kusikitisha sana,mishahara ya polisi,wa tz ni kichekesho,tu polisi ambao tunategemea walinde wananchi na malizao,
wanaishi,ktk flat ambazo, ni chafu hazina umeme,wala maji,sewerage system zimekufa, miaka nenda rudi,nazungumzia flats za buguruni,hata nyinyi ndugu zangu polisi,Hamulioni ni tatizo uchafu wa kutisha,nyinyi polisi familia zenu zinaishi
hapo,kwa usalama wa maisha yenye binafsi,na familia zenu.
Na hilo mnasubiri serikali ije,iwafanyie kila kitu,hivyo vibanda vya mkaa,vibanda vya vyakula jamani, m fike sehemu muone haibu,maflats ya polisi yote ni machafu,mrundikano wa vitu, kwenye vibaraza,aibu aibu,SERIKALI. Haiwezi kuja majumbani kwenu kuwafanyia usafi ni nyinyi wenyewe,na familia zenu,milipuko ya magonjwa kila mara, hamna macho,jirekebisheni.

MAONI KHUSU VITUO VYA POLISI,DAR,
NA SEHEMU ZINGINE...

Tunaelewa serikali haina pesa, ya kujenga vituo vya polisi,kila sehemu tunavyo vituo, vingine vimejengwa kwa nguvu za wananchi, Ila ni vichafu hamna huduma za vyoo hakuna maji,harufu mbaya.baadhi ya askari wana kauli mbaya sana,hapo vituoni rushwa rushwa, inasikisitisha zaidi,unapofika kwenye vituo vya polisi inabidi ununue karatasi za kukuandkia maelezo hivi serikali yetu inafanya nini?
khs hili imekuwanikawaida basi wapeni watu binafsi tenda wasasupply,stationaries muwalipe, Nje ya baadhi ya vituo vya polisi vya DAR,utadhani ni mnadani. vitu vimejazana ovyo magari yalichakongoroka,hamna utaratibu, wa wenye mali zao wakiisha maliza kesi wachukwe vitu vyao??

basi kuweni na utaratibu wa storage house,wenye vitu wachajiwe pesa, ni jambo la kusikitisha sana,hakuna cha bustani wala miti ni mrundkano wa vitu mbalimbali, jamani
tupende mazingira tunayofanyia kazi wapendwa.kwani ni sehemu ya masiha yetu,
Tatu wizara,zinazohusika na hili suala tunajuwa tuna magereza machache, wafungwa ni wengi,kwanini?
baadhi ya kesi ndogondogo ktk vituo vya polisi hao watuhumiwa wakishafikshwa mahamani,ziwepo sheria,za hao watu kufanya community services wasimamiwe na askari wasafishe,mitaro,wapake rangi majengo,watengeneze bustani,na baadhi ya kazi kwenye vituo vya polisi.badala ya kuwa na mrundikano wa watu magerezani,magereza mengi nchi yanakuwa nawafungwa wengi uwezo wa gereza ni mdogo,matokeo ni milipuko ya magojwa,vifo hivi vyote vingeweza kuepukika kama sheria zitapitiwa tena,za makosa madogo madogo na fine zake,jamani watanzania wenzangu tufike sehemu,tuangalie vinavyohusu nchi yetu,kwa kina, tunaweza kuwa na magari mazuri,nyumba nzuri ila tunaishi ktk mazingira machafu ya kutisha eweni watanzania wenzangu nchi inajengwa na wenye moyo safi na wazalendo wenye kupenda nchi yao siku zote samaki mmoja akioza ni wote watanuka,Mungu ibariki
Mdau K..

No comments: