Zitto Kabwe aula...
Na Tausi Mbowe.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini(Chadema),Kabwe Zitto(Pichani),ameteuliwa kuungana na Mtandao wa Wabunge Duniani,wanaoshiriki kuzuia na kulinda usalama wa wananchi.
Zitto anaingia katika mtandao huo wa wabunge wa kimataifa utakaokuwa hauko katika mfumo wa kichama na utakuwa ukijengwa na wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani ambao unafanya kazi kwa pamoja kitaifa na kimataifa.
Mtandao huo unaundwa chini ya Taasisi ya Mashariki na Magharibi ya Mtandao wa Wabunge (EWI),yenye makao yake makuu Brussels,Ubelgiji.
Wabunge hao watatarajia kuwa na mkutano Oktoba 8 mwaka huu, kwenye Bunge la Ulaya jijini Brussels,Ubelgiji.
Zitto ambaye ni mbunge kijana zaidi Tanzania anayewakilisha jimbo,alipata mwaliko kuhudhuria mikutano ya wabunge hao,ikiwa ni hatua ya kumkaribisha kufanya kazi katika mtandao huo.
No comments:
Post a Comment