Wednesday, July 29, 2009

Model ahukumiwa kuchapwa viboko 6 na Faini juu kwa kunywa Pombe hadharani, Malaysia.


image

Mahakama ya Sharia hapa Malaysia imemhukumu Mwanadada Kartika Sari Dewi Shukarno, 32 (Pichani) adhabu ya viboko 6 na faini ya Rm 5000 sawa na USD 1400 baada ya kupatikana na hatia ya kunywa pombe hadharani kwenye ukumbi wa starehe.

Kartika ambaye ni Mwanamitindo maarufu hapa Malaysia, Huku akibubujikwa na machozi alisema anatarajia kukata rufaa kwani kosa hilo kwake ni la kwanza lakini kwa mshangao wa wengi Kartika amesema kuwa ametupilia mbali suala la rufaa kwani ameonelea ni bora atumikie adhabu hiyo ili aweze kuendelea na maisha yake. “anasema rufaa inaweza kuchukua mwaka mmoja hadi miwili kusikilizwa jambo ambalo hana uhakika kama atashinda rufaa hiyo na pia litaendelea kumtesa moyo wake” alisema Mwanasheria wake.

image

Si kawaida kwa hukumu hii kupewa akina mama mara nyingi wamekuwa wakipewa wanaume lakini Hakimu huyo alisema kuwa ametoa hukumu hii ili iwe funzo kwa wengine waumini wa Kiislamu walio na tabia kama ya Kartika.

Ni majimbo matatu kati ya 14 nchini Malaysia yanayotumia kifungu hiki cha hukumu kaika Mahakama za Sharia.

Soma zaidi hapa, hapa na Hapa

No comments: