Tuesday, July 28, 2009

Wakala katika Skendo la Ununuzi wa Rada Adakwa nchini Uswizi


Shailesh Vithlani
Monday, July 20, 2009 6:00 AM
Wakala Shailesh Vithlani aliyetoroka Tanzania miaka mitatu iliyopita akiwa nje kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka katika skendo la ununuzi wa rada amekamatwa nchini Uswizi alikokuwa akijificha na atarudishwa Tanzania kujibu tuhuma zinazomkabili.
Vithlani alitoroka Tanzania miaka mitatu iliyopita akiwa nje kwa dhamana baada ya kushiriki katika kufanya uwakala wa ununuzi wa rada ya kijeshi ulioigharimu taifa la Tanzania mamilioni ya dola zaidi ya bei halisi ya rada hiyo.

Vithlani alifanya uwakala ambao uliifanya Tanzania itoe TSh bilioni 16 zaidi ya bei halisi katika ununuzi wa rada hiyo.

Awali taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza iligundua kuwa mkataba wa ununuzi wa rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya BAE Systems uligubikwa na rushwa kubwa.

Taasisi ya kupambana na rushwa PCCB iliomba msaada toka SFO kusaidia kukamatwa kwa Vithlani na kurudishwa Tanzania kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika ndani ya SFO na PCCB, Vithlani ameishakamatwa na atarudishwa Tanzania kujibu tuhuma zinazomkabili ndani ya wiki chache zijazo.

Mbali na Vithlani, raia sita wa Uingereza akiwemo mdau mmoja wa karibu wa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair wamehusishwa katika skendo hilo la rushwa katika ununuzi wa rada.

Vithlani alifanikisha dili la dola milioni 40 ( Zaidi ya Tsh. bilioni 40) kwa kufanya uwakala kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya BAE Systems katika ununuzi wa rada.

Vithlani inasemekana alipewa dola milioni 12 (zaidi ya TSh. bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha dili hilo na inasemekana aligawana pesa hizo na maafisa saba wa ngazi za juu katika serikali ya Tanzania.

Vithlani atarudishwa Tanzania kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya taratibu za kumkabidhi kwa serikali ya Tanzania kukamilika.


No comments: