Wednesday, July 15, 2009

balozi kijazi atoa somo kwa wanafunzi india
Balozi John Kijazi na Afisa ubalozi anayeshughulikia wanafunzi BW. Mwamunenge, wakitosi na uongozi Mpya uliokaribishwa nyumbani kwa Mh. Balozi kwa mazungumzo na chakula
Mh .Balozi Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na uongozi mpya wa TASA, sambamba na Afisa Ubalozi anayeshughulikia masuala ya wanafunzi

Balozi wa Tanzania nchini India Mh. John Kijazi amesisitiza mshikamano na umoja miongoni mwa watanzania waishio nchini INDIA, sambamba na kuheshimu sheria na taratibu za nchi ili kulinda heshima ya nchi ya Tanzania ambayo imekuwa na sifa kubwa ya kuheshimiana miongoni mwa wananchi wake kwa mataifa mengi Duniani.

Mheshimiwa Balozi KIJAZI, ameyasema hayo juzi usiku alipokutana na Uongozi Mpya wa wanajumuia ya wanafunzi wa Tanzania wanaoishi New Delhi, alioukaribisha nyumbani kwake CHATAPURI, RANDE- MOUHAN DRIVE, New Delhi, Ukaribisho ulioenda sambamba na chakula cha Usiku.

Bw. Kijazi amesema ubalozi ,wazazi na walezi wanatambua kuwa vijana wengi waliopo hapa New Delhi , India wanasoma na kuishi kihalali nchini hapa na kuwapa changamoto viongozi hao wapya wa TASA , kuhakikisha wanasimamia wenzao na kushirikiana na ubalozi katika kulinda heshima ya nchi yao.

Amewahimiza TASA kuimarisha umoja huo kwani ni njia pekee ya kuwaleta watanzania wengi karibu na kuuwezesha ubalozi pia kufahamu mengi kuhusu watanzania waliopo New Delhi na kusisitiza ushirikiano ulio wakaribu ambapo alisema" Kwa Balozi ni nyumbani kwa watanzania, cha muhimu ni kupeana taarifa wakati gani mnahitaji kukutana kwa shughuli zozote zenye lengo la kuwaleta watanzania karibu..".

Kwa upande wa uongozi Mpya ambao Mwenyekiti wake ni Bi Jennifer Sumi, akisaidiwa na katibu wake Privatus Kizito ulimshukuru Mheshimiwa Balozi kwa ukarimu wake na kuomba ushirikiano wa masuala mbalimbali, likiwemo la kuandaa BONANZA KUBWA ya watanzania waishio NEW DELHI inayotarajiwa kufanyika Mwezi SEPTEMBA mwaka huu, ambapo Mheshimiwa BALOZI alilipokea kwa furaha na kusisitiza liandaliwe kwa umakini na kuwasilishwa Ubalozini.

No comments: