Wednesday, July 15, 2009

Iran kuwekewa vikwazo zaidi




NEW YORK

Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na uhusiano wa kigeni, Benita Ferrero-Waldner, amependekeza Iran iwekewe vikwazo iwapo itakataa mazungumzo kuhusu uchaguzi wa rais uliompa ushindi rais Mahmoud Ahamadinejad. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, kamishna Benita Ferrero Waldner amesema jumuiya ya kimataifa inabakia kuungana na itatafakari kuiwekea vikwazo serikali ya mjini Tehran kuidhihirishia Iran kwamba haipaswi kuvuka mpaka. Wakati huo huo, maafisa wa polisi nchini Iran hapo jana walitumia gesi ya kutoa machozi kuuvunja mkutano wa waandamanaji takriban 250 karibu na chuo kikuu cha Tehran wanaopendelea mageuzi. Mgombea urais wa Iran aliyeshindwa, Mir Hossein Mousavi, amewatolea mwito wafuasi wake kuendelea na maandamano yao.

No comments: