ngeleja azindua mtambo wa kushindilia gesi asilia leo
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Yona Killagane wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliopo Ubungo jijini Dar
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (wa pili kulia) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Ethur Mwakapugi na kushoto kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiweka gesi katika gari wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Aliyesimama nyuma ya waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.
Mfanyakazi wa PanAfrican Energy (T) LTD akimuonyesha Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) jinsi ya kuweka gesi katika gari maalum wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Aliyesimama kulia kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akimsikiliza mkazi wa Ubungo Maziwa kuhusiana na maombi yao ya kulipwa fidia ili waweze kahama eneo hilo na kupisha ujenzi wa mitambo kupeleka gesi majumbani, kwenye taasisi na kwenye magari. Waziri Ngeleja alifika katika eneo hilo leo kwa ajili ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika. Picha na An na Nkinda wa Maelezo
No comments:
Post a Comment