Saturday, December 19, 2009

Majambazi yateka bar na kubaka mhudumu!

Kundi la majambazi wakiwa na silaha jana wamevamia glosari moja Kimara Suka, na kutembeza kichapo kwa wateja kisha kumteka mhudumu na kumla uroda bila idhini (kumbaka.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari tukio hilo limetokea jana saa 4 usiku, Kimara Suca.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa, majambazi hao baada ya kufika maeneo hayo walifyatua risasi hewani na kusababisha majirani wa eneo hilo kuanza kuhaha huku na kule kuokoa maisha yao.

Imedaiwa kuwa baada ya majambazi hayo kufyatua risasi hewani waliingia katika grossary hiyo na kisha kupora vitu mbalimbali ikiwemo simu za mikooni za watej, fedha.

Baada ya kufanya tukio hilo majambazi hayo ambayo idadi yake haikuweza kufahamika walitowekwa kwa kupita mabondeni huku wakiwa na mhudumu huyo ambaye walimbaka baadaye.

Kutokana na tukio hilo majirani walipiga kelele na ghafla polisi walifika eneo la tukio lakini hawakuweza kufanikiwa kuwakamata kundi la majambazi hayo ambayo idadi yake haikuweza kufahamika mara moja.

No comments: