Thursday, December 3, 2009

majembe yakabidhiwa rungu kusimamia huduma za safari

Mkuu wa Usalama barabarani James Kombe (pichani) akizungumza jijini Dar kuhusu utoaji huduma ya usafiri kupitia kampuni ya Majembe Auction Mart.

SUMATRA imeanzisha utaratibu mpya wa kuleta maboresho katika usafiri wa umma na kuondoa kero kwa wakazi wa jiji wa Dar.
Yania Kuanzia Desemba 1, 2009 Kampuni ya MAJEMBE AUCTION MART imekasimiwa kazi ya kusimamia, kufuatilia na kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa masharti ya leseni ya kusafirisha abiria katika jiji la Dar na kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo.

Mbali na kufanya kazi kwa karibu na Trafiki ambao ndio wanawajibu wa kusimamia sheria zote za nchi, Mamlaka itakuwa na utaratibu wake wa kufuatilia utendaji wao.

Wenye vyombo vya Usafiri, wafanyakazi wao, abiria na wananchi kwa ujumla wanaombwa kutoa ushirikianao wa hali ya juu ili kuleta maboresho yenye manufaa kwa umma.

No comments: