Tuesday, December 29, 2009

Bongo jamani !!!
Mdudu gani anatusumbua !!

Ankal kama nilivyokuahidi hali ya barabara ya Tarakea to Marangu hivi sasa si shwari. Yaani tumelazimika kusimama masaa sita baada ya barabara kuzuiliwa na Dar Express kama unavyoona ikiwa imejikita kwenye udongo, na kidogo tu iwamwage abiria zaidi ya hamsini waliokuwemo. Kama hiyo haitoshi likaja basi dogo la fuso hapo na kuziba barabara kwa kukwama na kusababisha usumbufu wa zaidi ya magari mia.
Picha na stori na Mdau Isaya Philip
Hapa ni Rombo Mkuu kilometa tatu tu kutokea Rombo kuelekea Marangu ambapo mdau Isaya Philip alilazimika kuacha vekesheni na kushirikiana na wadau kuwatoa wajenga nchi
zege halilali hapa....
Anko naninihii jionee hapo wakati nyie mnahangaikia barabara za gorofa na kusota kwenye foleni huko kwenu wenzenu wanahangaikia huku mitaa ya Tarakea barabara ya changalawe tu ili waondokane na adha hii ya kufanya kazi ngumu ya kusukuma magari kabla ya kazi zao za msingi
kimbembe Tarakea





No comments: