Friday, December 4, 2009

Benki ya EXIM yazindua akaunti ya Faida
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Beno Ndulu (kushoto) na Mwenyekiti wa Benki ya Exim, Yogesh Manek, wakiwa na mfano wa kadi ya ATM, mara baada ya kuzindua huduma mpya ya Faida Accont na kadi ya Faida, itakayomwezesha mteja wa benki hiyo kuchukua fedha katika benki yeyote ndani na nje ya nchi. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar usiku kuamkia jana
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Beno Ndulu (kushoto), akikata utepe kuzindua huduma mpya ya Faida Kadi itakayomwezesha mteja wa benki hiyo kuchukua fedha katika benki yeyote ndani na nje ya nchi. Kulia ni Mwenyekiti wa Benki hiyo Yogesh Manek. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar usiku kuamkia jana.

Profesa Ndullu akiwa na wakuu wa Exim bank

Benki ya Exim imezindua akaunti ya Faida ambayo itamuwezesha mteja kuchukua fedha kwenye mashine za ATM ya benki yoyote.

Mbali na faida hiyo gharama za kufungua akaunti hiyo ni chini na zinamuwezesha Mtanzania yoyote kumudu gharama za kufungua akaunti hiyo.

Akaunti hiyo inafunguliwa kwa shilingi 5000 tu.

Uzinduzi wa akaunti hiyo ulifanywa na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye aliipongeza benki kwa ubunifu wake na kuzishauri benki nyingine kuiga mfano huo.

“Tuwe wabunifu kama benki hii kwani kwa kufanya hivyo tutaweza kuwaletea Watanzania maendeleo kwa haraka,”

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Yogesh Manek aliwashauri wateja wa benki hiyo kufanya manunuzi kwa kutumia kadi hiyo kwani huduma hiyo ni bure.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,Bi. Sabetha Mwambenja alisema jana wakati wa uzinduzi , akaunti hiyo kwamba akaunti hiyo inawafaa zaidi wafanyabiashara ndogondogo na wa kati wafanyakazi wa sekta ya Umma na Binafsi na wanachama wa vikundi vya kuweka na kukopa.

“Kutokana na huduma zinazopatikana katika akaunti hiyo, akaunti ya Faida itawawezesha wateja wetu kujenga tabia ya kujiwekea akiba”alisema.

Alifafanua kwamba mbali na kufungua akaunti hiyo kwa shilingi 5000, , wateja wa benki hiyo pia wanapata kadi ATM ambayo inawawezesha kuchukua fedha hata nje ya nchi kwani imeunganishwa na mtandao wa kimataifa wa fedha wa MasterCard .

Alisema Faida akaunti hiyo ni pamoja na kupata huduma za hundi.

Alisema mbali na Faida inajenga mahusiano mazuri na wateja wake kwani mteja anapopata kifo cha ajali analipwa bima ya shilingi milioni 1 bure.

“Tuwe wabunifu kama benki hii kwani kwa kufanya hivyo tutaweza kuwaletea Watanzania maendeleo kwa haraka,”


No comments: