Saturday, December 19, 2009

Mzungu mwingine ammwagia maji machafu Askari

Lile sakata la raia wa kizungu kumtemea askari mate likiwa bado halijapoa.....baada ya kufukuzwa nchini,raia mwingine wa Afrika Kusini amemdhalilisha askari mkoani Arusha kwa kummwagia maji machafu.

Katika tukio hilo lililotokea juzi, raia huyo wa Afrika Kusini, Gesina Susanna Hayes, alimmwagia maji machafu askari huyo aliyekuwa akilinda Benki ya Barclays iliyopo katika majengo ya TFA na kisha kumdondoshea kapu la matusi ya nguoni.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio,baada ya tukio hilo, askari huyo PC Sengerema mwenye namba G.1757, alimdhibiti Hayes na kumfikisha katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini humo na kufunguliwa jalada namba AR/RB/8591/09 kabla ya kufikishwa mahakamani.

Baada ya kufikishwa mbele ya mahakama,mzungu huyo alishindwa kujitetea, hivyo Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo kumhukumu kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka.

No comments: