Friday, December 18, 2009

Hasheem Ateuliwa Timu Ya Taifa Ya Kikapu Bongo

(pichani),mtanzania ambaye wengi wanamtarajia kuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi maarufu ya mpira wa kikapu nchini Marekani(NBA), ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji 21 walioteuliewa kuchezea Timu ya Taifa ya mpira wa kikapu nchini Tanzania kwa upande wa timu ya wanaume.Pia wanawake 20 wameteuliwa kuunda timu ya taifa kwa upande wa wanawake.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Tanzania(TBF),Lawrence Cheyo, timu hiyo ya wanaume itakuwa chini ya makocha Bahati Mgunda na Evarist Mapunda wakati ile ya wanawake itakuwa chini ya makocha Salehe Zonga na Pascal Nkuba

No comments: