Saturday, December 19, 2009

Meya akunjwa shati,jasho zamtoka!
Kiumbe cha kiume ambacho hakikuweza kufahamika jina,kilimkunja shati na kumtukana matusi ya nguoni Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Salum Londa,alipokuwa akitoa shukrani kwa wananchi wake wa jimbo la Kawe..kwa kuweza kuwapa ushindi ktk uchaguzi wa serikali za mitaa uliokwisha katika siku za karibuni.

Sinema hilo lilianza,pale jamaa huyo alipoanza kutoa maneno yake ya kejeli baada ya kumuona Londa anawaaga wananchi wake baada ya kumaliza kutoa shukrani zake.

Baada ya kuona hivyo mwanaume huyo aliinuka kwa hasira sehemu aliyokaa na kwenda kuziba mlango ili Londa asipate pa kupita .

''Wewe mheshimiwa mimi nakuona kama umepungukiwa kwanza auna kitu unachokifanya hapa Kawe kazi yako ni kudanganya wananchi tu '' alidai mwananume .

Wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuona hivyo walimshika mwanaume huyo na kumpeleka katika kituo cha polisi cha Kawe .

Naye, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa mzimuni akiongea baada ya sekeseke hilo alisema hawamjui mtu huyo ila walikuwa wanamsikia tu kuwa anapenda kumfanyia fujo Londa wakati akiwa anawahutubia wananchi mikutanoni.
chanzo darhotwire.

No comments: