Tuesday, December 8, 2009

SAJILI NAMBA YAKO YA VODACOM SASA!
Vodacom Tanzania inapenda kuwakumbusha wateja wake wote kuwa zoezi la uandikishaji wa namba za simu lililoanza Julai Mosi mwaka huu bado linanaendelea na litakwisha tarehe 31 Disemba 2009. Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia.

1. Swali: Ni kwa nini nisajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Ni ili niweze kujilinda na kuilinda namba yangu kutoka kwa wale wanaotumia vibaya huduma za mawasiliano.
2. Swali: Ni wapi ninapoweza kuisajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Fika kwenye Vodashop au wakala wa M-PESA yoyote yule aliye karibu na wewe ukiwa na kopi (kivuli) ya moja ya vitambulisho vifuatavyo;

I. Kitambulisho cha kupigia kura
II. Pasi ya Kusafiria
III. Kitambulisho cha Pensheni (NSSF, PPF, LAPF, PSPF)
IV. Leseni ya Udereva
V. Kitambulisho cha kazi pamoja na barua ya Mwajiri
VI. Kitambulisho cha Shule au Chuo
VII. Barua iliyopigwa muhuri kutoka kwa Mtendaji Kata pamoja na picha ndogo

3. Swali: Je kuna gharama yoyote ya kusajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Hapana, usajili ni BURE
4. Swali: Je zoezi hili la kusajili namba za mitandao ya simu limeanza lini na litakwisha lini?
Jibu: Zoezi hili lilianza Julai mosi mwaka huu na litakwisha Disemba 31 mwaka huu.
5. Swali: Je ni nini kitatokea iwapo nitakuwa sijasajili namba yangu ya Vodacom baada ya Disemba 31 mwaka huu?
Jibu: Kulingana na maelezo kutoka Tume ya Mawasiliano, mteja husika atajulishwa na kisha namba yake itafutwa kutoka kwenye orodha ya namba za simu.
6. Swali: Je ninaweza nikasajili namba ya mteja mwingine?
Jibu: Ndiyo, unaweza kusajili namba ya mteja mwingine iwapo tu unayo maelezo yote yanayotakiwa na Tume ya Mawasiliano.
7. Swali: Je ninatakiwa niisajili tena namba yangu ya Vodacom hata kama nimeshajisajili na huduma ya M-PESA?
Jibu: Hapana, huhitaji kuisajili tena namba yako iwapo umeshajisajili na huduma ya M-PESA na umeacha nakala ya kitambulisho chako. Iwapo haukuacha nakala ya kitambulisho basi itakubidi uache nakala ya kitambulisho chako chenye picha.
8. Swali: Je ni idadi ya namba ngapi za Vodacom ninazoweza kuzisajili?
Jibu: Hakuna idadi ya namba unazotakiwa kuzisajili. Unaweza kusajili namba nyingi kadri uwezevyo.
9. Swali: Je kuna usiri wa kiasi gani kwa habari nitakazozitoa wakati wa kusajili namba yangu?
Jibu: Makapuni yote ya simu yanatakiwa kwa mujibu wa sheria kutunza kwa usiri mkubwa habari zote zitakazotolewa na wateja wake.


Pamoja daima.
Vodacom Tanzani
a

No comments: