Tuesday, December 29, 2009

basi a meridian express lapata ajali mkata jioni jana

wananchi kijiji cha Mkata mkoani Tanga wakiangalia

basi la Meridian lililogongana na lori jioni jana sehemu hizo

Mie ndo natoka vekesheni Roitoktok huko Kenya mpakani mwa Tanzania, nimepita njia ya Tarakea, yaani haifai. Baadaye kidogo ntakutumia taswira za huko.
Hapo juu ni ajali nimeikuta sehemu za Mkata mkoa wa Tanga ambapo basi la Meridian limegongana na lori. Dereva wa Meridian kajitahidi sana kuokoa maisha ya abiria kwani lori lilihama njia na dereva wa Meridian akasave kidogo kwa kuingia kwenye reserve ya barabara.
Hadi naondoka saa kumi jana hamna aliyekufa ila majeruhi walikuwa kibao na polisi walikuwa hawajafika.

Mdau Isaya Philip

No comments: