Wednesday, December 30, 2009

libeneke la culinary chamber lanukia, kuzinduliwa mwaka mpya
mambo ya kuchonga chonga pia
yatakuwepo ktk blog ya culinary chamber
Asalaam alaykhum ankal Kadidi,

Wajina, blog yetu ya CULINARY CHAMBER itazaliwa rasmi tar 1/1/2010. Hivi sasa article za awali zinamaliziwa pamoja na picha baadhi. Imani yangu ni kuwa wataalamu wa fani hii watachangia kwa moyo mmoja ili wadau wote wapenda misosi waweze kufaidika kwa utaalamu wa mapishi mbali mbali yatakayoporomoshwa. Nnaimani ushirikiano utakua mzuri ili tuboreshe blog yetu. Mwanzo mgumu ila penye nia pana njia tutafika tu kwa juhudi na uchakarikaji.

Pokea picha hizo ambazo nilibahatika kushiriki pia mashindano ya finger foods ambayo lengo haikua kupata mshindi ila ni kubadilishana ujuzi toka kwenye vyuo mbali mbali vya culinary duniani vyenye ushirikiano wa pamoja toka nchi za Croatia, USA, Uk, France, Italy, Malaysia , Indonesia, India, Korea, China, Singapole, German, Austria, Swistzerland, Netherland, spain na Belgium.
Picha za vyakula na habari zaidi watazipata ktk blog ya Culinary Chamber.
Baada ya mashindano hayo jioni ilikua ni bonge la party wanafunzi waliochukua kozi ya general hotel management na mambo ya matukio walitoa perfomance safi yenye ladha ya mataifa yao ilikua super sana ankal michuzi.
Ila kubwa kuliko yote ni pale nilipooona bendera ya taifa langu imepanda juu kama heshima ya mshiriki toka Tanzania. ohhhhhh.... nilihisi machozi kunidondoka kwa furaha.

Ndugu zangu nawaomba sana sana tushirikiane. Shule hii ni bure wala hakuna gharama yeyote kwa hiyo yeyote mwenye ujuzi atoe, msijifiche. Huu ndio wakati muafaka wa kubadilishana utaalamu kwani hakuna anaejua zaidi. Wote tunajua kiasi kwa hiyo tukichanganya maarifa inakua safi mambo yanakamilika na kunoga au vipi kaka misupu? hahahahhahaa
HAPPY NEW YEAR TO ALL !
nashukuru sana kwa maoni yenu yote
nayaheshimu sana mungu awabariki.

Chef Issa
Chef Issa akiwa na Chef Leonard ambaye ni senior lecturer wa culinary wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan Univeristy

usiku baada ya mashindano ilikua ni bonge la party na bendera za nchi washiriki zote zilipandishwa. Cheki bendera yetu inavyowaka.

No comments: