Tuesday, December 8, 2009

allan lucky wa EATV alonga
Allan Lucky wa EATV

SWALI: Wazo la kuanzisha show za mashuleni kwa ajili ya wanafunzi limetoka wapi?
ALLAN: Idea ya show ya wanafunzi, ni idea iliyokuwepo muda mrefu kichwani mwangu, na nikasema kama nikipata nafasi ya kuwa kwenye tv au radio, moja ya show ambazo nitazianzisha ni show ya wanafunzi, nilipopata nafasi ya kujiunga na EATV, nikawa katika mlengo tofauti kidogo, nikafikiria sana show za muziki. Lakini nikiwa hapo nikakutana na wenzangu ambao walikuwa na idea kama hizo mfano Cynthia Lymo, ambao tayari walishaanza kuzitekeleza, basi mimi nikaonekana kuwa ni perfect person for it. Na obvious, mimi ndio niliyetoa jina la show, skonga. So, after that, we started working on our idea.

SWALI: Unafikiri kati ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki, ni wanafunzi wa wapi ni wajanja kimasomo na katika nyanja nyinginezo?
ALLAN: Duh, hilo swali ni tricky kiaina. Anyways, huwa nachat sana na wanafunzi kutoka Uganda na Kenya, na tanzania pia, nchi zote tatu ni wajanja, wanazidiana tu katika nyanja mbalimbali. Kiukweli, wanafunzi wa Kenya, wako much more exposed kwa maisha ya watu tofautitofauti, na wako more knowledgeable kulinganisha na tanzania na uganda, sisemi kwamba tanzania hawako hivyo, but ni wachache sana ambao wako hivyo. Asilimia kubwa ni wanafunzi wa kawaida tu ambao general knowledge walio nayo wao ni ndogo sana ukilinganisha na wenzao wa kenya au uganda. Lakini Tanzania mi nadhani wanafunzi wana vipaji sana, kama serikali ikiamua kulitazama hilo suala kwa makini, watathibitisha haya maneno yangu.


Kwa mahojiano kamili
BOFYA HAPA

No comments: