Friday, September 5, 2008

Wasabato Masalia watimuliwa Tena
Uwanja wa Ndege wa Mw.Nyerere
Dar Es Salaam..

Pichani ni Baadhi ya waumini Wasabato,wanaojitambulisha kama'Masalia'baada ya kutimuliwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, ambako wamekuwa wakipiga kambi kwa imani ya kunyakuliwa hadi Ulaya bila pasipoti,tiketi,visa na taratibu zingine za usafiri wa kimataifa.
---
*Polisi yatoa onyo la mwisho kwa Wasabato Masalia


KUNDI la waumini wa Dhehebu la Waadventista Wasabato Masalia, kwa mara ya tatu limesambaratishwa na askari wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kurudi tena uwanjani hapo huku wakiwa wameongezeka idadi yao kutoka 17 hadi kufikia 51.
Wasabato hao masalia,walifika katika uwanja huo mnamo saa 2:00 asubuhi huku wakiwa na mabegi yao tayari kwa safari wakisema:"Bwana alikuwa amewaambia tena kuwa jana ilikuwa ndio siku ya kuondoka na kuelekea nchi za Ulaya kuhubiri injili."Bofya na Endelea....>>>>>

No comments: