Monday, March 31, 2008

Taarifa kwa Vyombo vya Habari !

***Fomu za tuzo za Vinara Zatolewa
---------
Fomu za ushiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo za Vinara wafilamu Tanzania 2007/8 zimeanza rasmi kutolewa jana katika vituombalimbali nchini ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kutolewa kwa tuzohizo.Tuzo hizo zitakazotolewa kwa mara ya kwanza nchini, zimeandaliwa nakampuni ya One Game Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya BiaTanzania (TBL) kupitia bia yake ya dovu Power Malt.
Mratibu tuzo hizo, Khadija Khalili, amesema kuwa, kutokana na sababuzilizo nje ya uwezo wao, fomu hizo zilichelewa kutoka kwa tarehe yaawali hivyo kusababisha kuongezwa kwa muda wa kurejeshwa fomu nakupokea filamu zitakazoshiriki katika tuzo hizo hadi Aprili 18 badalaya Machi 31 kama ilivyotangazwa awali.Alisema watengenezaji wa filamu nchini wanakaribishwa kutuma nakala zafilamu zilizotengenezwa kati ya Januari 2007 hadi Machi 31, 2008, kwaajili ya kuwania tuzo hizo.
Khalili alisema kuwa, jopo la majaji litakutana baada ya Aprili 18kuchagua watakaowania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2008.Alisema fomu za kushiriki kuwania tuzo hizo zinapatikana katika vituovilivyotangazwa awali ambavyo ni ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) kwa Omari Mayanga, pia zinapatikana kwa wasambazaji wa filamuambao ni Wananchi Wote, GMC, Kapico na Game First Quality."Fomu zilizojazwa na nakala ya filamu iliyopo kwenye mfumo wa VCD naDVD zitumwe kwenye ofisi za BASATA zilizopo Ilala Bungoni jijini Dares Salaam au ofisi ya One Game Promotion," alisema.
Vipengele vitavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo kuwa ni FilamuBora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora waMwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, MuigizajiBora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Mwongozaji Sinema Bora wa Mwaka,Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu, Mtunzi Bora waFilamu, Filamu Bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizii Bora wa kike(supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Borakwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora waFilamu ambao wote watapata tuzo na zawadi.Pia itatolewa tuzo yaheshima kwa wale waliotoa machango wao kukuza sanaa nchini

No comments: