Monday, March 31, 2008

Hitimisho...


Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akitazama muda kabla ya kufunga rasmi
kikao cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) kilichofanyika Butiama kwa siku mbili na kumalizika jana.kabla ya kufunga kikao hicho Rais kikwete alifafanua zaidi sababu za kufanyika Butiama na alikiri kuwa, kingefanya maamuzi mazito ambayo hayatahusu mageuzi ya kisera wala kiitikadi.Nalisema hili kwa sababu wapo watu wanaotumaini au wenye hofu kuwa hapa Butiama, kutatokea tamko la kurudia tena kutaifisha mali na kuziweka njia kuu za uchumi mikononi mwa dola. Wapo pia wanaodhani tutatoa tamko la kulirudisha nyuma gurudumu la mageuzi ya kisiasa yaliyoleta demokrasia ya vyama vingi na uhuru mkubwa wa watu kutoa maoni yao," alisema.
Kikwete alifafanua kuwa, kikao hicho kingetatafakari hali ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama katika chama na taifa na kuwa katika kuzungumzia mambo hayo, yapo masuala makubwa yatakayojitokeza na kufanyiwa maamuzi.

No comments: