Monday, March 31, 2008
Ndio Maana Naipenda Bagamoyo!
Bagamoyo jana alasiri. Pichani ni hotel ya Millenium.
Ufukwe wake umetulia. Pichani ni jana Jumapili mchana. Mpaka mwisho wa upeo wa macho yako humwoni mtu. Kutoka hapa unaweza kutembea kwa miguu kufuata ufukwe hadi kijiji cha Kaole, huko kuna magofu ya kale. Bagamoyo ni mahali pazuri, gharama zake ni za chini ukilinganisha na sehemu nyingine za kitalii. Ukiwa na shilingi elfu tatu mfukoni Bagamoyo utapata chai ya asubuhi, chakula cha mchana na cha jioni. Na bado utafika beach kuogelea na kupunga upepo. Kutoka Dar hadi Bagamoyo unaweza kufika kwa Daladala, nauli haizidi elfu na mia tano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment