Na Michael Uledi, Dodoma
MPANGO wa kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya Jimbo katika majimbo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umeanza kuonyesha dalili za kukwama baada ya baadhi ya wafadhili kuuona unalenga kukinufaisha kisiasa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema hayo jana wakati akimkabidhi ofisi Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Stephen Wassira.
Kutokana na wafadhili kutoa kasoro hiyo, Pinda alisema kuwa, unahitaji msukumo wa ziada ili kufanikisha kuanzishwa kama ilivyokusudiwa na serikali.
"Kuna hili suala la Constituent Development Fund (CDF) (mfuko wa maendeleo ya jimbo), donors (wafadhili) hawataki hata kusikia na mwisho kuna mmoja akanieleza kuwa wanaona kuwa unalenga kuinufaisha CCM kisiasa,� alisema Pinda.
Vilevile, alimweleza Wassira kuwa, mpango wa ujenzi wa ofisi za wabunge unakabiliwa na wakati mgumu kutokana na kukosa fedha za kutosha.
Pinda, alisema Sh1bilioni, zilitengwa na serikali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi za wabunge, lakini fedha zilizotolewa zinatosheleza kujenga ofisi sita.
Alisema hadi anakabidhi ofisi TAMISEMI kwa Wassira, ilikuwa imepatiwa Sh165 milioni, ambazo zinaweza kujenga ofisi za wabunge sita, nne bara na mbili Zanzibar kwa kuwa kila ofisi moja hujengwa kwa Sh25milioni.
" Mradi huu unalenga kuwapatia waheshimiwa wabunge ofisi za majimbo yao kwa madhumuni ya kusogeza huduma na kukuza demokrasia,� alisema na kuongeza kuwa: " Mwaka
2007/2008 zimetengwa shilingi bilioni moja kwa ajili ofisi 40 kwa bara 32 na nane Zanzibar. "
Hata hivyo, alisema mradi huo, unakabiliwa na uhaba wa fedha za utekelezaji kwa kuwa kiasi cha Sh25 milioni zilizotengwa kwa ajili ya ofisi moja, hazitoshi kwa kuwa mazingira ya majimbo ya uchaguzi yanatofautiana.
Katika hatua nyingine; Pinda alimtahadharisha Wassira kuwa atakumbana na changamoto nyingi kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuwa na ofisi Dodoma na Dar es Salaam.
Alisema itategemea na maamuzi yake kama waziri, ingawa alitoa angalizo kuwa, kauli yake isichukuliwe kuwa anawataka kurudi Dar es Salaam.
Serikali mwaka jana ilikubali kuanzisha mfuko huo wa maendeleo ya jimbo ambao ulitarajiwa kuanza rasmi, mwaka huu wa fedha.
Akiwasilisha taarifa ya mwelekeo wa makadirio ya bajeti kwa mwaka 2007/08 kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi Juni mwaka jana, Waziri wa Fedha wa wakati huo, Zakia Meghji, alisema serikali ilikuwa tayari imekamilisha taratibu za kuanzisha.
Alisema mfuko huo, ungeanza rasmi katika bajeti ya serikali ya 2008/09 baada ya kufanyika maandalizi ya msingi kufikia uanzishwaji wake.
Ili kupata uzoefu wa nchi zenye Mfuko huo, timu ya wataalam ilitembelea nchi za Kenya na Zambia, mwezi Aprili, mwaka jan
No comments:
Post a Comment