ULINZI umeendelea kuimarishwa katika eneo la mtambo wa maji wa Ruvu wilayani hapa Mkoa wa Pwani kufuatia kuwapo kwa tishio la kuwekwa sumu, ambalo lilitolewa wiki iliyopita na wanaodhaniwa kuwa ni wafanyakzi wa DAWASCO.
Gazeti hili jana lilishuhudia magari zaidi ya matano yakiwa na askari polisi yakifanya doria katika eneo hilo kwa kushirikiana na askari wa usalama wa taifa.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Henry Salewi alisema kuwa, jeshi hilo linaendesha ulinzi wa hali juu katika maeneo ambayo hata hivyo kwa ajili ili kuepuka kuvuruga upelelezi.
Kwa upande wke Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dk Christine Ishengoma amewataka wananchi kutokuwa na wasiwasi na maji wanayotumia kwa sasa baada ya Serikali kuimarisha ulinzi katika eneo la mtambo huo.
Baadhi ya wakazi wananchi mkoani Pwani, waliomba serikali kushughulia kikamilifu tishio hilo.
Wiki iliyopita wafanyakazi DAWASCO katika mtambo wa Ruvu chini walitishia kuweka sumu kwenye mtambo mkubwa unaosafirisha maji kwenda mkoani Pwani na Dar es Salaam kwa lengo la kuwaua watumiaji endapo uongozi wa shirika hilo hautawarejesha kazini wafanyakazi watano waliofukuzwa kazi.
No comments:
Post a Comment