Saturday, March 29, 2008

Mambo Yote Butiama...


Rais jakaya kikwete akiwapungia wananchi wa Butiama kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa kumbukumbu ya Joseph Kazurira Nyerere ulioko Butiama kuongoza mkutano wa Kamati kuu ya CCM jana.Kushoto ni katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba na wapili kushoto ni mkamau mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa.

Rais jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ukumbi wa kumbukumbu ya Joseph Kazurira Nyerere, Butiama jana kuongoza mkutano wa Kamati Kuu ya CCM. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mama Maria Nyere, katibu Mkuu wa CCM , Yusufu Makamba, Makamu wa Rais, Dr. Ali Mohammed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, John Malecela na Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha.
-----------------
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara.Kikao hicho kimeanza tu muda siyo mrefu baada ya Rais Kikwete kuwa amewasili Butiama tayari kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM .

Kikao cha NEC kinaanza kesho ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika kijiji ambako alizaliwa Baba wa Taifa na mwanzalishi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Rais Kikwete aliwasili Butiama kwa barabara akitokea Mwanza ambako ndege yake ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza mapema asubuhi na akaamua kusafiri kwa gari kwenye Musoma.Mjini Mwanza, mamia ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake, walijitokeza kwa wingi, katika baadhi ya sehemu za jiji hilo mvua ikiwa inanyesha, kumshangilia Rais wakati msafara wake ukikatisha mitaa ya jiji hilo kuelekea Musoma.

No comments: