Saturday, March 29, 2008

mnaambiwa bongo tambarare hamsikii

mnaambiwa bongo tambarare hamsikii
Bro Safari,

Napitia uani mzee kwani kupitia mbele inashindikana itabidi labda unielekeze kwa haraka nini nakosea. Inawezekana ni setting kwenye computer yangu. Eee bwana nina issue hapa naomba iwekwe hadharani lakini tumia jina hili MPIGANIA HAKI.

Ninaandika masikitiko yangu kwa TRA Dar es alaam namna wanavyorudisha nyuma jitihada za kuinua uchumi na badala yake wanatengeneza mazingira ya rushwa. Sijui kama tutashinda vita dhidi ya mafisadi.

Nikiwa mwanafunzi huku abroad nimejibana kutuma gari huko nyumbani kwa mzee wangu lisaidie familia. Gari ni isuzu used nimelinunulia Japan kwa gharama nafuu kabisa. Kuepuka usumbufu wa kipengele cha kuingiza gari lisilozidi miaka 10, basi nilinunua gari ya mwaka 1999.
Gari ilisafirishwa toka Japan mwezi wa 11 mwaka jana na kuingia bongo mwishoni mwa desemba 2007. Jamaa zangu huko home walifuatilia kulitoa na jamaa wa TRA wakasema lilipiwe milioni 5 kwa maelezo eti ni la kifahali. Hatukubishana, pesa ilitafutwa ikalipwa.
Nikapata taarifa eti TRA wametupiga faini ya milioni 2 zaidi kwasababu wamegundua gari ni ya mwaka wa nyuma imeandikwa kwenye mikanda tofauti na ilivyoelezwa kwenye papers.
Mimi nikahisi kuna harufu ya dhuruma hivyo nikawaambia ndugu zangu wasilipe fine wafuatilie kiundani. Wakawasiliana na kampuni inayoingiza magari ya isuzu toka Japan. Jamaa wakawapa taarifa ya maandishi kuwa gari used zinazonunuliwa Japan zinafungwa vifaa vipya kuondoa vichakavu.
Kuna uwezekano mkanda uliofungwa ukawa mwaka tofauti na manufacture date ya gari. Barua ilipelekwa TRA kwa wahusika basi mpaka leo Michuzi inapigwa dana dana. Wanasema wiki hii eti kuna sekretari TRA aliipoteza barua haikuweza kuingia kwa mkubwa, hivyo wakahitaji copy ambayo tulikuwa nayo waiingize kwa mkubwa.
Sijui itachukua muda gani na gari iko bandarini muda wote huo.


Nimeona uozo huu niuanike hadharani ili kama kuna yoyote anayeweza kunisaidia anisaidie.

MPIGANIA HAKI

No comments: