Monday, March 31, 2008

Makontena ya mbao kwenda China

WIZARA ya Mali Asili na Utalii imezuia shehena ya makontena kumi ya mbao katika Bandari ya Dar es Salaam ambazo zilikuwa zisafirishwe China baada ya wizara hiyo kuyatilia mashaka makontena hayo.
Sambamba na kuzuia shehena hiyo ya mbao, wizara hiyo inamchunguza afisa wa wake aliyekagua na kuidhinisha mbao hizo, ili zisafirishwe licha ya kuwepo kwa aina mbalimbali za mbao. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga alisema makontena hayo yamezuiliwa baada ya kubaini kuwa kuna udanganyifu uliofanywa na mfanyabiashara mmoja ambaye hakumtaja jina kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea,Habari hii na James Magai.

No comments: