Friday, March 28, 2008
ismail aden rage ni mtu huru sasa !!!
MAHAKAMA ya Rufaa jana imemsafisha Rais wa klabu ya Moro United Ismail Aden Rage baada kushinda rufaa ya hukumu iliyotolewa wakati akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) na sasa TFF miaka sita iliyopita.
Majaji Damian Lubuva, John Mroso na Mbarouk S. Mbarouk wamefuta hukumu ya miaka mitatu jela iliyotolewa mwaka 2005 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam na baadaye kuthibitishwa na Mahakama Kuu.
Imebainika kuwa hakukuwa na vielelezo vya kutosha kuonyesha kuwa Rage alitenda kosa alilohukumiwa nalo. Wakati wa kusikiliza rufaa hiyo, mwendesha mashitaka alikiri kuwa hatia aliyokutwa nayo Rage kutokana na makosa mawili haikuwa sahihi.
Makosa aliyokuwa akikabiliwa nayo ni yanayomhusisha kuiba Sh milioni 1 kutoka Salvation Army ya jijini Dar es Salaam ambako timu ya Taifa iliweka kambi kwa ajili ya maandalizi na michezo ya kimataifa na Sh 400,000 alizodaiwa kuwalipa posho wachezaji. Habari kamili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment