Kiu Ya Kusoma!
Leo nilikuwa kijijini Imalutwa, Kilolo, Iringa. Hicho ni kijiji anachotoka mwenzetu Michael Mlowe. Nikiwa hapo kijijini niliweza kuongea na vijana kadhaa wakiwamo hao wanaonekana pichani. Hapo kijijini kuna club ya FEMA ya kujisomea na kujadiliana. Niliwapa majarida ya ' Si Mchezo' yanayotolewa na FEMA. Kama inavyoonekana, hilo lilikuwa jambo kubwa kutokea kwa leo. Wote wakazama kwenye kusoma na kuangalia picha. Akatokea kijana kwa jina la Salum kutoka kijiji jirani cha Uhambingeto, yeye naye alitaka nimpe majarida hayo aende nayo kijijini kwao. Nikamwambia, kwanza aende akaanzishe kikundi cha FEMA CLUB akishirikiana na wenzake wa Uhambingeto. Kijana Salum alinitazama machoni na kuniuliza; " Braza hivi kikundi maana yake nini?"
Nilipoanza kumfafanulia ndipo nilipozidi kuona umuhimu wa mimi na wengine kukutana na vijana kama Salum, kukaa nao chini na kuongea, iwe kijijini Imalutwa au Uhambingeto.Ni wajibu wetu. Asante sana Maggid kwa picha na maelezo yako Muruwa !!
No comments:
Post a Comment