Saturday, March 29, 2008

TAFAKURI

Kuna mdau mmoja Baraka Karashani kanipa hii:
ANGALIA MZUNGUKO WA SAA YAKO.
Kuna mtu mmoja alifariki dunia na akaenda kwa Mungu,alipofika akakuta saa za ukutani nyingi sana zimetundikwa. Akauliza "Hivi hizi saa ni za nini huku?" Akajibiwa na Askofu mkuu aliyemkuta huko, "Kila saa ina dhambi za kila Binadamu,ikizunguka mara moja ina maana ametenda dhambi mara moja".
Yule jamaa akauliza "mbona hii hapa imesimama ni mbovu? Akaambiwa hiyo ni ya mama Theresa, na inamaanisha kuwa hakutenda dhambi kabisa ndio maana imesimama.
Jamaa ikabidi aulize tena, "hivi saa ya Edward Lowasa na Ballali iko wapi kati ya hizi?" akajibiwa, "ya hao ndugu iko ofisini kwa Bwana Yesu mwenyewe maana anaitumia kama feni kwa jinsi inavyozunguka mara nyingi na kwa kasi."

2 comments:

thotha said...

see it herehop over to these guys great post to readimp source this pagehe has a good point

Anonymous said...

q7f86d5q74 q6r43a6s19 n0c59x7a57 v8p06r4p29 u0j53p6r28 a4x36n5o79