
Pichani ni watoto wadogo ambao vichwa vyao ni vidogo kupindukia kwa
mujibu wa mdau Mpoki Bukuku aliyenishushia habari hii hivi punde.
Mama Sophia Lipeleta mkazi wa Nachingwea Mtwara akiwa na watoto wake walemavu pichani na kueleza kuwa alikuwa na watoto saba wa aina hiyo sasa wamebaki hawa watatu baada ya wengine kufa.

Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida.
-------
Wadau kwa niaba ya mdau Mpoki Bukuku aliyeniletea habari hiii hivi punde ni kwamba
kuna watoto wa ajabu wamezaliwa kama muonavyo pichani ambao ni wa Bi Sophia Lipeleta mkazi wa Nachingwea Mtwara ambaye alifika ofisi za gazeti la mwananchi hivi punde kwa nia ya kuomba msaada kwa wasamaria wema kwani watoto wake hawa hawawezi kuongea japokua wana umri mkubwa na kuomba kama kuna mtu atapenda kufanya utafiti anaweza kuwafanyia na kujua tatizo, lakini wako Dar na hawana chakula wala pa kulala kwani hivi sasa wanalala stendi za mabasi. Mama yao anaomba msaada wa hali na mali,nami nimeona niungane na ndugu yangu Mpoki Bukuku kuomba msaada kwa wasamaria wema ili tuwasaidie watoto hawa.
Kwa wale wenye nia ya kuchangia watoto Hawa Mnaweza
kumpigia Simu Mpoki Bukuku kupitia Number hiii
+255222450878 au Fax +255222450886
E-mail:mpokibukuku@yahoo.co.uk