Roy bukuku afariki dunia
Prodyuza nguli wa muziki hapa bongo aliyetambulika kwa jina la Roy Bukuku amefariki jana huko Mkoani Mbeya alikozaliwa,kwa taarifa zaidi tuendee za msiba huo na mengine tutajulishana hapa hapa Jamvini.
Roy mpaka anafariki alikuwa prodyuza wa studio za G 2 Records ,na alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga kinanda.Ambapo mnamo mwaka 1985 akiwa nchini Uingereza alishiriki mashindano ya kupiga chombo aina ya piano na kuibuka mshindi na kujinyakulia tuzo iliotambulika kwa jina la SEVEN OAKS THREE ARTIST FESTIVAL.Pamoja na ujuzi wa muziki Roy pia alikuwa mtaalamu wa mambo ya Kompyuta, na menginyo .
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amin
No comments:
Post a Comment