JK atunuku kamisheni maafisa wa jeshi leo
Amiri Jeshi Mkuu JK akikagua gwaride la heshima wakati wa sherehe za kuwatunuku kamisheni maafisa wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli leo. Jumla ya wanafunzi 22 kutoka Botswana walikuwa miongoni mwa maafisa wapya waliohitimu leo
JK akiwa pamoja na mgeni wake Rais wa Botswana Lt.Gen.Seretse Khama Ian Khama wakati wa sherehe za kuwatunuku kamisheni maafisa wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli leo.Jumla ya wanafunzi 22 kutoka Botswana walikuwa miongoni mwa maafisa wapya waliohitimu leo
Amiri jeshi mkuu JK akimpongeza na kumzawadia Mwanafunzi bora katika mafunzo ya maafisa wa jeshi Luteni Usu Israel Ibrahim Mwashala, wakati wa sherehe za kuwatunuku maafisa wapya wa jeshi waliohitimu mafunzo ya mwaka mmoja katika chuo cha jeshi TMA kilichipo Monduli,mkoni Arusha

JK na Khama waongelea mustakabali wa Zimbabwe
Na Mwandishi Maalum, Arusha
Tanzania na Botswana zimeelezea masikitiko yao kuhusu kukwama kwa utekelezaji wa makubaliano ya mgawanyo wa madaraka baina ya vyama vya ZANU-PF, MDC-T na MDC-M nchini Zimbabwe.
Tanzania na Botswana zimeelezea masikitiko yao kuhusu kukwama kwa utekelezaji wa makubaliano ya mgawanyo wa madaraka baina ya vyama vya ZANU-PF, MDC-T na MDC-M nchini Zimbabwe.
Nchi hizo mbili zimesema kuwa hatua zozote za kuzidi kucheleweshwa kwa utekelezaji wa makubaliano hayo haitumikii na wala kujali matakwa na maslahi halisi ya wananchi wa Zimbabwe.
Nchi hizo mbili zimeelezea msimamo wao huo katika taarifa ya pamoja iliyotolewa leo, Jumanne, Oktoba 21, 2008, mjini Arusha mwishoni mwa ziara ya siku mbili ya Rais Seretse Khama Ian Khama nchini Tanzania.
Taarifa hiyo inasema kuwa marais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na Khama wa Botswana pamoja na kufurahishwa na hatua ya kufikiwa kwa makubaliano baina ya vyama hivyo Septemba 15 mwaka huu, bado wamesikitishwa na ukweli kuwa utekelezaji wa makubaliano hayo umekwama.
Viongozi hao wawili wameutaka uongozi wa kisiasa katika Zimbabwe kuchukua hatua za haraka na za lazima kuhakikisha utekekelezaji wa makubaliano hayo ya mgawanyo wa madaraka na hasa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa haraka iwezekanavyo.
Viongozi hao wamesema kuwa wananchi wa Zimbabwe wanastahili kupewa nafasi ya maelewano mapya, nafasi ya kutibu makovu ya kitaifa, na pia nafasi ya kujenga upya taifa lao.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa katika mazungumzo yao ya faragha na ya Kiserikali viongozi hao wamepata nafasi ya kujadili masuala mengine ya kimataifa na yale yanayohusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wameelezea kuridhishwa na kiwango cha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili na kuelezea matumaini yao ya kuuboresha uhusiano huo.
Pia viongozi hao wawili wamewaelekeza mawaziri wao wa mambo ya nje kufufua upya Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo, ili kuiwezesha tume hiyo kuwa chombo imara zaidi cha kuendeleza uhusiano wa karibu zaidi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii miongoni mwa watu wa nchi hizo mbili.
Mwishoni mwa ziara yake, Rais Khama ambaye ameondoka nchini leo mchana kurejea nyumbani, amemshukuru mwenyeji wake na wananchi wa Tanzania kwa ukarimu wao wakati wa ziara hiyo.
Rais Khama pia amemwalika Rais Kikwete kutembelea Botswana, na Rais Kikwete amekubali mwaliko huo ambao utafanyika kwenye tarehe zitakazokubaliwa kupitia mikondo ya kidiplomasia.
Luteni Jenerali Khama ambaye aliwasili nchini jana, Jumatatu, Oktoba 20, 2008, pamoja na mwenyeji wake leo wameshiriki kwa pamoja katika sherehe ambako Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Rais Kikwete ametoa kamisheni kwa maofisa wapya 155 kundi la 48 katika Chuo cha Maafisa wa Kijeshi (TMA) Monduli, mkoani Arusha.
Maafisa 22 wa kike kutoka Botswana walikuwa miongoni mwa maafisa hao wapya waliotunukiwa kamisheni kwenye sherehe hiyo.
Miongoni mwa maofisa wa Botswana waliofuatana na Rais Khama ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa P.T.C. Skelemani, Waziri wa Ulinzi, Sheria na Usalama D.N. Seretse, na Kamanda wa Jeshi la Botswana Luteni Jenerali T. C.H. Masire.
No comments:
Post a Comment