Friday, October 24, 2008

manispaa singida yazika maiti waliyopewa kimakosa, nako manispaa ya temeke shughuli ni pevu bado.
kaburi likifukuliwa
kaburini ilikozikwa maiti kimakosa
maiti ikiondolewa kaburini
maiti ikiingizwa mochuari


Picha na habari na
Mdau Hudson Kazonta
wa HabariLeo

WATU saba wanahojiwa na Polisi kuhusu mtafaruku ulioibuka baada ya tukio la wafanyakazi wa Manispaa ya Singida kupewa kimakosa na kwenda kuuzika mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa katika hospitali ya Singida kwa muda.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa Celina Kaluba alisema tayari Polisi inawahoji watu saba kuhusu tukio hilo na watakaobainika kuhusika kwa uzembe huo watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Katika tukio hilo lisilokuwa la kawaida, Manispaa ya Singida iliuzika mwili wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Mwanahamisi Omari (39) mkazi wa kijiji cha Kinyagigi katika halmashauri ya wilaya ya Singida, ambaye alifariki Oktoba 16 katika hospitali ya Nkungi kwa matatizo ya uzazi.

Mwili wa Mwanahamisi ulipelekwa katika hospitali ya mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa siku moja kabla ya kwenda kuzikwa siku inayofuata.

Akizungumzia suala hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Dk. Aubrey Mushi, alisema hali hiyo imesababishwa na uzembe wa muuguzi wa zamu pamoja na wafanyakazi kutoka Manispaa wenye majukumu ya kuzika miili ya watu iliyokosa ndugu.

Alisema katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo kulikuwa na maiti moja ya mahabusu mwanaume aliyejulikana kwa jina la Mwamanela Makumbi (32) ambaye alifariki Oktoba 16 mwaka huu.
---------------------------------------------------
Manispaa ya Temeke nako....
Wakati huo huo, utata umezidi kugubika suala la kukataa maiti ya marehemu Bakari Omari (30), baada ya ndugu zake kuendelea kudai si ya ndugu yao, licha ya jana kutambua nguo za marehemu walizokuwa wamemvalisha walipompeleka kumhifadhi katika Hospitali ya Manispaa ya Temeke Dar es Salaam.
Omari alifariki dunia Ijumaa iliyopita na kuzikwa kimakosa katika makaburi ya Temeke Wailes na mwili wake ulifukuliwa kwa amri ya mahakama juzi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Manispaa hiyo zilidai kuwa jana kuliitishwa kikao cha Mkurugenzi wa Manispaa, Mkuu wa Wilaya, viongozi wa juu katika manispaa hiyo pamoja na ndugu wa marehemu hao wawili waliochanganya maiti hizo.
Maiti nyingine ni ya marehemu aliyetambuliwa kwa jina la Yusuf Anthony ambaye hata hivyo hakuwahi kuzikwa na maiti yake iko hospitalini Temeke.
Katika kikao cha jana, inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Kihato alikitumia kujadiliana na ndugu wa Omari kuhusiana na alama ya ndugu yao pamoja na kuwaonyesha nguo.
Kihato inaelezwa kuwa aliwataka ndugu wa Omari kuchukua maiti iliyofukuliwa kuwa ni ya ndugu yao, jambo ambalo ndugu hao walikaidi na kumtaka kuwapa nafasi ili wafanye kikao cha familia.
kwa habari zaidi za mkasa huu nenda

No comments: