Thursday, October 23, 2008

posta J3 palikuwa hapatoshi kwa machinga kudadadeki

Mwingine huyu hapa,yaani J3 ilikuwa ni kukamata kamata tu kwa kwenda mbele
Huyu nae alikuwa anajiuzia maji yake yuko chini ya ulinzi


Na wewe ndio husikii eeh,unajificha nini haya chomoka hapo ulipo fasta


"Haya panda huko araaa"!




Masikini ..! mwenyewe katoka home asubuhi smati,akirudi nguo zake zote zimechanwa chanwa na askari wa jiji



"Haroo songesha haraka , tunawakataza msifanye biashara zenu sehemu zisizoruhisiwa hamsikii"!
Wameishafanya varangati lao hao wanatambaa kuwasaka wengine,ukumbuke kwenye karandiga hilo pichani wameswekwa machinga kibao na bidhaa zao




J3 mchana maeneo kadhaa kati kati ya jiji la Dar kulikuwa na hali ngumu kwa machinga,hali hiyo imesababishwa na askari wa jiji kwa kuvamia na kuanza kukakamata kamata kila aliyekaa kihasara hasara na anayefanya biashara sehemu isiyoruhusiwa.Ilikuwa ni vuta nikuvute kwani machinga nao hawakutaka kukubali kukamatwa kirahisi na bidhaa zao walizokuwa nao.
Nilijaribu kuzungumza na muhusika mkuu wa operation hiyo ya askari wa jiji akaniambia kuwa hivi karibuni katikati ya jiji kumezuka vibaka wengi ambao wamekuwa wakiporwa porwa vitu/mali zao,"hivyo tumeamua kupitisha msako huu angalau kupunguza hii hali ambayo imeanza kujitokeza kwa kasi" alisema mkubwa huyo huku akiendelea kutoa amri kwa askari wake

No comments: