Thursday, October 16, 2008

Ajali ajali !!

ajali ilitokea wami ilisababishwa na fuso iliyopakia machungwa na mafenesi kutoka mkoani Tanga. Gari hiyo ilianguka baada ya kushindwa kupanda mlima kuelekea mto wami .
Ajali ilitokea maeneo ya vigwaza baada ya fuso kugongana na TAnker la mafuta
Ajali hii ilitokea mwishoni kabisa mwa wiki iliopita haya ni maeneo jirani na mzani kibaha maili moja!!


Picha hizi zikionesha foleni katika daraja la wami. Habari nilizozipatikana toka kwa dereva wa lori hilo inasemekana alipakia chumvi na baada ya kuvuka daraja la wami na kuanza kupanda kilima ghafla gari lake aina ya scania 113,360 iliishiwa upepo na kuanza kurudi nyuma ma katika harakati za kuokoa mali ya mteja na gari ndipo alipokunja kona na muonekano wa gari ukawa 7 . hivyo kufunga barabara kwa muda wa saa 5 . Poleni sana kwa wale wahanga na pia shukrani mdau kwa picha hizi tamu na pia kwa ufundi wako wakukamata picha !!!

No comments: