Saturday, October 18, 2008

albino magic team waendelea na tizi la nguvu, wapigwa taffu na EATV
mtangazaji wa kipindi cha michezo cha EATV patrick nyembela akitoa zawadi ya mpira kwa nahodha wa Albino Magic Team wakati wa mazoezi yao ocean road. mpira huo umetolewa na msamaria mwema ambaye hakutaka jina lake litajwe. patrick ametoa wito kwa wasamaria wema wengine kujitokeza kuisaidia timu hii ya aina yake kwa hali na mali kwani kama wanavyoonekana hawana vifaa vya michezo na pia hujinyima hata kula ili kusevu nauli ya kuhudhuria mazoezi kila siku.
patrick nyembela na nahodha wa Albino Magic Team wakitoa tano kwa msamaria aliyewapa zawadi ya mpira
tizi likiendelea kwa sana
hapo wakipata vifaa vya uhakika lazima maximo apate salamu siku moja
kikosi cha Albino Magic Team kikila pozi na mwalimu wao (kulia). azma kuu ya kuanzishwa kwa timu hii ambayo ni ya kwanza hapa nchini pengine na kwingineko duniani ni kupata fursa ya kujiweka fiti na pia kuhamasisha wananchi kuondokana na fikra potofu dhidi ya wadau albino, badala ya kukaa tu na kungoja misaada.
kikosi hiki kesho kinatarajiwa kuungana na jumuiya ya albino katika maandamano ya kupinga unyanyasaji wa maalbino na pia kuishinikiza serikali ichukue hatua madhubuti na za kudumu dhidi ya unyanyapaa pamoja na mauaji ya kikatili ya albino.
maandamano hayo, yanayotarajiwa kupokewa na JK viwanja vya karimjee kesho asubuhi, yataanzia mnazi mmoja.



No comments: