Friday, October 24, 2008

ZENYE MAKOSA DALADALA TU?


Askari wa kikosi cha usalama barabarani leo walikuwa bize na ukamataji wa magari yenye makosa mbalimbali kama walivyonaswa na kamera yetu leo mchana maeneo ya Sinza Bamaga jijini Dar es Salaam.
Lakini mwandishi wetu alishuhudia gari nyingi zilizokamatwa zilikuwa ni zile zinazofanya shughuli za daladala.
Shuhuda mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe katika mtandao huu, alitonya kuwa hiyo inatokana na waendesha daladala hao kuwa wepesi wa kutoa mshiko ili waachiwe. Kama ni kweli hiyo noma.

No comments: