Saturday, October 18, 2008

Msafara Wa Pinda Una-Pinda Kona!


ona hapa ndipo anaponipungia mkono !~!
Jumatano mchana nikiwa njiani kurudi Iringa nilikutana na msafara wa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kilomita kadhaa kuvuka daraja la Mto Ruaha Mkuu, mpakani mwa Iringa na Morogoro. Ulikuwa ukielekea Morogoro. Mheshimiwa alinipungia mkono kama inavyoonekana kwenye moja ya picha hizo. Labda alishangaa kuona raia wake yuko porini akiwa amebeba kamera! Na hakika hatujawahi kukutana wala hanifahamu.

No comments: