Mugabe Ajipendelea
MGOGORO wa Zimbabwe unaweza kuchukua sura mpya baada ya Rais Robert Mugabe, kushindwa kutekeleza matakwa ya wapinzani katika mgawanyo wa madaraka katika Baraza la Mawaziri.
Mugabe na kiongozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai, wa Chama cha MDC, walifikia makubaliano ya kugawana madaraka katika mkataba uliosainiwa Septemba 15 mwaka huu.
Chini ya makubaliano hayo, ilitarajiwa kuwa Mugabe atawaachia MDC baadhi ya nafasi nyeti katika baraza la mawaziri lakini hilo halijafanyika.
Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa Mugabe ametangaza baraza la mawaziri, huku nafasi nyeti nyingi akizitenga kwa ajili ya Chama chake cha ZANU-PF.
Hatua hiyo imepingwa vikali na MDC, ambayo imebainisha kuwa uamuzi wa Mugabe unayaweka makubaliano ya kugawana madaraka njia panda.
Kwa muda mrefu tangu kusainiwa kwa makubaliano hayo, pande hizo zimekuwa zikivutana kuhusiana na mgawanyo wa wizara, kiasi cha kumlazimisha msuluhishi wa mgogoro huo, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, kurejea kuendelea na kazi ya usuluhishi.
Lakini, Mugabe na chama chake wanasisitiza kuwa orodha hiyo ya mawaziri imekubaliwa na vyama vyote, wakiwamo wapinzani.
Naibu Waziri wa Habari kutoka ZANU-PF katika baraza lililopita, Bright Matonga, aliiambia BBC kuwa mgawanyo wa madaraka uliofikiwa ni wa haki kwa vyama vyote.
Katika mgawanyo huo, ZANU-PF itakuwa na wizara 14 zikijumuisha wizara za Ulinzi, Mambo ya Nje, Sheria, Serikali za Mitaa na Habari.
Chama cha upinzani cha MDC cha Tsvangirai kimetengewa wizara 13 zikiwamo Katiba na Bunge, Uchumi, Mipango na Uwekezaji, kazi, Michezo, Utamaduni, Sayansi na Maendeleo ya Teknolojia.
Tawi jingine la MDC lililo chini ya uongozi wa Mutambara limetengewa wizara za Elimu, Viwanda na Biashara.
Hii inamaanisha kuwa ZANU-PF itakuwa na wizara 14 wakati wapinzani kwa pamoja watakuwa na wizara 16.
Matonga alisema kuwa nafasi ya wizara ya fedha bado haijapangiwa mtu yeyote.
Hata hivyo, msemaji wa MDC, Nelson Chamisa, aliitaja orodha hiyo kuwa ni ya kiburi cha ZANU-PF ambayo itasababisha makubaliano yao kuwa tete.
“Jana tulikubaliana tumwite tena msuluhishi, Thabo Mbeki, kwa sababu tulikuwa hatujaelewana. MDC haikubaliani na orodha iliyotangazwa, ni upuuzi,” alisema.
Moja kati ya matarajio ya MDC ni kupatiwa dhamana ya kuendesha wizara inayohusika na masuala ya polisi, hasa iwapo ZANU-PF ikiwa inaongoza wizara ya ulinzi.Mugabe na kiongozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai, wa Chama cha MDC, walifikia makubaliano ya kugawana madaraka katika mkataba uliosainiwa Septemba 15 mwaka huu.
Chini ya makubaliano hayo, ilitarajiwa kuwa Mugabe atawaachia MDC baadhi ya nafasi nyeti katika baraza la mawaziri lakini hilo halijafanyika.
Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa Mugabe ametangaza baraza la mawaziri, huku nafasi nyeti nyingi akizitenga kwa ajili ya Chama chake cha ZANU-PF.
Hatua hiyo imepingwa vikali na MDC, ambayo imebainisha kuwa uamuzi wa Mugabe unayaweka makubaliano ya kugawana madaraka njia panda.
Kwa muda mrefu tangu kusainiwa kwa makubaliano hayo, pande hizo zimekuwa zikivutana kuhusiana na mgawanyo wa wizara, kiasi cha kumlazimisha msuluhishi wa mgogoro huo, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, kurejea kuendelea na kazi ya usuluhishi.
Lakini, Mugabe na chama chake wanasisitiza kuwa orodha hiyo ya mawaziri imekubaliwa na vyama vyote, wakiwamo wapinzani.
Naibu Waziri wa Habari kutoka ZANU-PF katika baraza lililopita, Bright Matonga, aliiambia BBC kuwa mgawanyo wa madaraka uliofikiwa ni wa haki kwa vyama vyote.
Katika mgawanyo huo, ZANU-PF itakuwa na wizara 14 zikijumuisha wizara za Ulinzi, Mambo ya Nje, Sheria, Serikali za Mitaa na Habari.
Chama cha upinzani cha MDC cha Tsvangirai kimetengewa wizara 13 zikiwamo Katiba na Bunge, Uchumi, Mipango na Uwekezaji, kazi, Michezo, Utamaduni, Sayansi na Maendeleo ya Teknolojia.
Tawi jingine la MDC lililo chini ya uongozi wa Mutambara limetengewa wizara za Elimu, Viwanda na Biashara.
Hii inamaanisha kuwa ZANU-PF itakuwa na wizara 14 wakati wapinzani kwa pamoja watakuwa na wizara 16.
Matonga alisema kuwa nafasi ya wizara ya fedha bado haijapangiwa mtu yeyote.
Hata hivyo, msemaji wa MDC, Nelson Chamisa, aliitaja orodha hiyo kuwa ni ya kiburi cha ZANU-PF ambayo itasababisha makubaliano yao kuwa tete.
“Jana tulikubaliana tumwite tena msuluhishi, Thabo Mbeki, kwa sababu tulikuwa hatujaelewana. MDC haikubaliani na orodha iliyotangazwa, ni upuuzi,” alisema.
Chini ya makubaliano hayo, Mugabe ataendelea kuwa rais wa nchi hiyo, huku Tsvangirai akiwa waziri Mkuu.
Mgogoro wa Zimbabwe umesababisha kuzorota kwa uchumi pia na kupanda kwa mfumko wa bei. Juzi ilitangazwa kuwa kiwango cha mfumko wa bei kimefikia asilimia milioni 231.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema kuwa unahitaji kiasi cha dola milioni 140 kwa ajili ya kununua chakula cha msaada kwa ajili ya wananchi wa nchi hiyo ambao wanakabiliwa na njaa. Kiwango hicho kitatosheleza kuwapatia wananchi hao chakula katika kipindi cha miezi sita ijayo
Habari kwa Hisani Ya Tanzania Daima

No comments:
Post a Comment