Tuesday, October 21, 2008

harakati kupinga mauaji ya albino zapamba moto

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi,Maalbino ,wakati alipopokea maandamano ya kulaanani ukatili na mauaji ya maalbino,yaliyofanyika katika viwanja vya ukumbe wa Karimjee jumapili asubuhi.
albino na wanaharakati wa kupinga ukatili dhidi ya albino wakiandamana

Mbunge wa kuteuliwa anayewakilisha maalbino, Al Shaimaa John Kwegyir akiteta jambo na JK wakati wa hafla ya kuzindua na kuichangia taasisi ya Goodhope Star Foundation ambayo itatetea na kutoa huduma kwa maalbino nchini,iliyofanyika katika hoteli ya Movenpick. Katika harambee hiyo iliyoendeshwa na JK zaidi ya shilingi 16.3/m zilikusanywa.Rais Kikwete alitoa jumla ya shilingi milioni mbili na nusu 2.5/m kama mchango wake kwa taasisi hiyo.
ujumbe kwenye mabango unaeleza hisia za wanaharakati hawa na albino wakiwa maandamanoni


No comments: