Tuesday, October 28, 2008

Gorila Wa Congo Kwenye Mikono Ya Gen. Nkunda

Imeripotiwa jana kuwa majeshi ya waasi mashariki mwa Congo- Kinshasa yakiongozwa na Jenenerali Nkunda yameitwaa milima ya Virunga ambayo pia ni hifadhi ya taifa yenye gorilla wengi. Walinzi wa hifadhi wamekimbia na gorilla hao wako hatarini kushambuliwa kwa kuwa katikati ya pande mbili zinazopigana. Mwaka jana mwezi Agosti majangili walivamia hifadhi hiyo na kuua idadi kubwa ya gorilla kama inavyoonekana pichani na ililipotiwa katika blogu hii. Mgogoro wa Congo hadi sasa umepelekea mauaji ya watu milioni 5, hata hivyo hivyo, mara zote ulimwengu unasahau idadi ya gorilla waliopoteza maisha bila hatia katika mgogoro huo.

No comments: