Jose chameleone avunjika miguu
Msanii mashuhuri wa Uganda Jose Chameleone inaelezwa kuwa amevunjika miguu yote miwili baada ya kuanguka toka ghorofa ya tatu ya hoteli moja kubwa ya kitalii a-taun mwishoni mwa wiki.
Habari za uhakika toka kampala zinasema Chameleone, ambaye alikuwa bongo kwa ziara ya maonesho kadhaa, hivi sasa amelazwa hospitali jijini humo kwa matibabu.
Uhakika wa nini kilimsibu msanii huyo bado unatafutwa lakini habari za awali zinadatisha kwamba alikuwa ameamka kitandani kwake na kuelekea kwa kutembea huku akiwa ndotoni (sleep walking, nadhani kwa kiinglishi) kwenye balkoni ya chumba chake na kula mwereka.Habari zaidi tega sikio hapa hapa Jamvini
Pichani ni msanii Chamelione alipokuwa kwenye onesho mojawapo hapa jijin Dar.
Blog ya kadidi2 inamwombea kwa Mungu msanii huyo matibabu mema na arejee katika afya njema
No comments:
Post a Comment