BREKING NYUUUZZZZZZZ
askari wa kituo kidogo cha feri wakila doria sehemu lilipotumbukia na kuzama canter feri, huku mv kigamboni ikila mzigo na kufanya safari zake za kigamboni na kurudi kama kawaida. chini ni wapiga mbizi wakiwa katika harakati za kulifuga kamba hilo gari
GARI AINA YA CANTER LIMETUMBUKIA SASA HIVI PALE FERI BAADA YA KUSHINDA KUPANDISHA KIMLIMA CHA KUTOKEA KWENYE PANTONI UPANDE WA MJINI.HAKUNA MTU ALIYEDHURIKA NA AJALI HIYO KWANI DEREVA, ALIYEKUWA PEKE YAKE WAKATI AKITOKA KWENYE PANTONI, ALIAMUA KUCHUMPA BAADA YA KUONA GARI IMEGOMA KUSIMAMA, LICHA YA KUWEKEWA KIGOGO NA UTINGO WAKE ALIYEKUWA NJE YA GARI.
HADI GLOBU YA JAMII ILIPOKUWA INAONDOKA ENEO LA TUKIO MILANGO YA SAA SITA KASOROBO HIVI SAA ZA BONGO, JUHUDI ZA KULITOA HILO GARI KATIKA MAJI ZILIKUWA ZINAENDELEA AMBAPO WAZAMIAJI WALIKUWA WAKIPIGA MBIZI KULIFUNGA KAMBA KABLA YA KULIOPOA, BAADA YA ABIRIA KUPUNGUA NA MUDA WA FERI KUMALIZIKA USIKU WA MANANE.
HII SI AJALI YA KWANZA KUTOKEA MAHALI HAPO KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI, NA MAISHA KUPOTEA. ISHUKURIWE SAFARI HII DEREVA ALIKUWA SHAPU. SABABU YA KUSHINDWA KUPANDA KILIMA KWA GARI HILO HAIJAJULIKANA NA INASEMEKANA HAIKUWA NA MZIGO MKUBWA
No comments:
Post a Comment