hata tanga magofu yanakula nyundo kwa zamu


Sio Dar tu majumba makuu kuu yanakula nyundo kupisha majengo mengine mapya na ya kisasa,la hasha hata kwa wagosi wa kaya nako kazi ni moja tu,kusafisha majumba yalijichokea na kuleta mapya yatakayoleta sura iliochangamka na ya kuvutia katika mji wa Tanga.Tatizo katika ubomojai wamajumba haya ni kwamba wameyabomoa kidogo sijui kuwatisha wenye nyumba/wapangaji waondoke halafu wameyaacha hivyo hivyo,kutokana na hali ya hayo majengo baadhi ya wakazi wa tanga wameanza kulalama kwamba kama wahusika wameamua kuyabomoa majumba hayo basi wayabomoe na si kuyaacha kama yanavyoonekana pichan kwani yanatishia usalama wa wapita njia
No comments:
Post a Comment