MTUHUMIWA wa makosa ya mauaji,Rashid Kibati (35),Baada ya kutolewa chooni akidhibitiwa na askari kanzu na askari wa kikosi cha zimamoto mkoa wa Morogoro.Picha Mali ya gazeti la Mwananchi na Mdau Mpoki Bukuku.
--------------
SHUGHULI za Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro jana zilisimama kwa saa tatu baada ya mshitakiwa kutumbukia chooni kwa nia ya kujiua kukwepa kesi ya mauaji inayomkabili.
Mshitakiwa huyo, Rashid Salumu(35)mkazi wa Kijiji cha Gonja,Tarafa ya Turiani,Wilaya ya Mvomero alifanya kituko hicho akiwa mahabusu kabla ya kesi yake kutajwa.
Inadaiwa kuwa mahabusu huyo alimuomba askari aliyekuwa zamu Pc Elias kwenda kujisaidia na askari huyo akamsindikiza mpaka kwenye mlango wa choo hicho na kumuacha aingine peke yake.
Akari huyo aliendelea kusubiri nje,na alipoona mshtakiwa hatoki alipopata wasiwasi na kuamua kuingia ndani,ndipo alipopigwa na butwaa kwa kushindwa kumuona.Bofya na Endelea....>>>>>
No comments:
Post a Comment