Wednesday, September 10, 2008

Miss Universe Tanzania 2008 atoa
Msaada wa Sh1.5 Milioni kwa
Wagonjwa jijini Dar es Salaam.
Miss Universe Tanzania 2008,Amanda Ole Suluul akikabidhi kifurushi cha Zain chenye zawadi anuwai kwa mgonjwa,Farida Pius aliyejifungua watoto pacha,Kulwa na Doto katika Hospitali ya Mwananyamala,alipozuru hospitalini hapo jijini Dar leo kwa lengo la kusaidia wagonjwa.Katikati ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania,Tunu Kavishe.Zain ilimdhamini Amanda.
Miss Universe Tanzania 2008,Amanda Ole Sulul akikabidhi vifurushi vyenye zawadi kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala,Suleiman Muttani,alipozuru hospitalini hapo, jijini Dar leo kwa lengo la kusaidia wagonjwa.Katikati ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe.Zain ilimdhamini Amanda.
-----------
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain inayotoa huduma katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati,imemdhamini mrembo anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2008, Amanda Ole Sulul kwa lengo la kusaidia shughuli mbalimbali za jamii.

Ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kauli mbiu yake ya A Wonderful World(Ulimwengu Maridhawa),Zain imemdhamini Amanda Ole Sulul anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2008 linaloandaliwa na Kampuni ya Compass Communications,kwa kumwezesha kuandaa kazi mbalimbali za hisani ikiwa ni pamoja na kusaidia watoto na akina mama wajawazito waliolazwa katika wodi za hospitali za Serikali.

Hospitali mojawapo ambayo mlimbwende huyo alizuru na kufanya kazi za hisani kusaidia jamii jana ni ya Mwananyamala ambako Amanda alinunua bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na khanga, nguo,mashuka,manukato na mengineyo kwa ajili ya watoto na akina mama wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

Pia Amanda amejitolea kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati mrembo huyo alipozuru hospitalini hapo leo,Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania,Tunu Kavishe, alisema:"Zain kama kampuni tunawajibika kusaidia jamii ambayo imekuwa ikituunga katika biashara yetu.

No comments: